Habari namba moja ya Afrika sasa hivi ni Robert Mugabe kuondolewa madarakani Zimbabwe ambapo bado Jeshi la nchi hiyo limekua kwenye maongezi ya kuharakisha Mugabe kuachia madaraka.
Wakati Chama Tawala cha ZANU PF kinachotaka Makamu wa Rais aliefutwa kazi mwezi huu kuchukua nafasi ya Mugabe kikitarajia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mugabe Jumanne ya November 21, imeelezwa kwamba Makamu wa Rais huyo aliekua amekimbia nchi, anarejea Zimbabwe.
Taarifa ya CNN imeeleza kwamba Makamu huyo wa Rais Emmerson Mnangagwa anarejea Zimbabwe akitokea mafichoni alikokimbilia baada ya kufutwa kazi ambapo pia kauli iliyotolewa saa kadhaa zilizopita na Jeshi la Zimbabwe, Robert Mugabe atakutana na Mnangagwa ili kufanya mazungumzo.
Wananchi wa Zimbabwe wamejitokeza kupaza sauti kwa maandamano mitaani wakionyesha furaha yao ya Mugabe kuachia nchi ambapo Afisa Mwandamizi wa chama tawala ZANU PF Paul Mangwana, amesema Rais Mugabe (93) anatuhumiwa kumpa madaraka makubwa mke wake, kitendo ambacho ni ukiukwaji wa Katiba na pia hana tena uwezo wa kuongoza nchi.
ULIPITWA? BOSS ALIEMPA DR. SHIKA DILI LA TANGAZO AONGEA “ILIKUA NIKATE TAMAA”