Ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu ateuliwe kushika nafasi ya Urais baada ya kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Nchi ya Zambia Michael Sata, Guy Scott amesimamishwa uongozi wa chama cha Patriotic Front kutokana na kukiuka katiba ya chama hicho.
Scott ameshutumiwa na Chama hicho kwamba amekuwa akitumia vyombo vya habari kujitangaza yeye zaidi na kujitenga na agenda za chama chake na amekuwa akifanya maamuzi mengi bila ya kushirikisha chama chake.
Mbali na adhabu hiyo bado Scott anaendelea kuwa Rais wa Zambia mpaka atakapochaguliwa Rais mwingine kwenye uchaguzi utakaofanyika mwakani, japo yeye hatokuwa na nafasi ya kugombea kiti hicho tena.