Zanzibar ni moja kati ya sehemu za Tanzania zinazovutia kwa utalii duniani, kuna mengi ya kujifunza kutoka Zanzibar, ukarimu, upendo wa watu na mapenzi ya kufanya ibada kwa kiasi kikubwa. Ukiachana na hayo January 13 wakati tunasubiria kutazama fainali ya 10 ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, nimekutana na jambo jingine la upendo.
Zanzibar kuna utaratibu ambao huenda sehemu nyingi za mikoa ya bara unaweza usiukute, baadhi ya mitaa ya visiwani hapo, kuna utaratibu wa kiungwana, kama ni mpita njia na huna fedha ya kununua maji ya kunywa, kwa Zanzibar sio tatizo, kuna baadhi ya nyumba nje zimetengeneza vifaa vya kupozea maji kwa ajili ya mpita njia na mtu yoyote ambaye anaweza kuhisi kiu na kunywa, kuna vikombe vya kunywea maji na unaweza kupata huduma hiyo saa 24.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.