Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Ummy Mwalimu amesema moja ya jambo lililowachelewesha kuleta muswada wa bima ya afya ni suala la kuunganisha huduma za wazee na bima ya afya.
Mh. Ummy amesema hayo leo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza liloulizwa na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Dk. Oscar Ishengoma Kikoyo liliosema “Pamoja na nia njema ya serikali kutoa matibabu bure kwa wazee wetu zoezi zima limegubikwa na ukiritimba, Je, serikali haioni busara kuainisha vitambulisho vinavyotolewa kwa wazee na bima ya afya ili wazee wetu wapate tiba stahiki?”.
“Suala la kuunganisha huduma za wazee na bima ya afya ni jambo moja lililotucheleshwa kuleta muswada wa bima ya afya kwenye bunge lako ilikuwa kuweka utaratibu kama huo, pale ambapo serikali italeta muswada wa bima ya afya itaweka utaratibu ambao utaondoa hizi changamoto za matibabu bure kwa wazee” Waziri Ummy