Leo imetangazwa kuanza msimu mpya wa burudani kupitia chaneli mbali mbali ndani ya king’amuzi chake cha StarTimes, Katika msimu huo mpya wa burudani kutakuwa na maudhui tofauti tofauti kuanzia tamthiliya mpya, michezo pamoja na vipindi vipya vya Burudani.
Kupitia chaneli ya ST Swahili wataanza kuonyesha msimu mpya wa Coke Studio Africa kuanzia jumapili hii tarehe 10 Februari. Kipindi cha Coke Studio Africa ni moja ya vipindi vya Burudani vinavyopendwa zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, afisa mahusiano wa kampuni hiyo Samwel Gisayi ameelezea zaidi.
“Tunazidi kujipambanua kama Wafalme wa burudani za familia, na Coke Studio Africa ni kipindi kinachoweza kuangaliwa na familia nzima, muziki wa kuvutia ambao haupatikani sehemu nyingine. Sasa jumapili hii ya tarehe 10, kuanzia saa 2:00 Usiku hadi saa 3:00 Usiku, msimu mpya wa Coke Studio Africa utaanza kuonekana rasmi”>>> Samwel Gisayi
“Tena kwa bahati nzuri mwaka huu Coke Studio Africa kuna wasanii watano kutoka Tanzania tena wote wanafanya vizuri ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Yupo Nandy, Harmonize na Rayvanny kutoka WCB, JUX na Mimi Mars. Burudani kubwa sana kwa wateja wetu kuanzia wikendi hii”,
Mbali na Coke Studio, pia wametangaza ujio wa tamthilia mbili ambazo zitaanza mwanzoni mwa mwezi wa tatu
“Tuna tamthilya mbili mpya ya kwanza inaitwa Suluhu ambayo ni ya Kiswahili, ina waigizaji maarufu kama Muhogo Mchungu, Korongo na marehemu Mzee Majuto, yenyewe itaanza tarehe 1 mwezi wa tatu. Nyingine ni tamthiliya ya Kihindi inayoitwa ‘Warris’ ambayo imeingiziwa sauti za Kiswahili hapa hapa Tanzania, Monalisa na Godliver ni miongoni mwa waliongiza sauti katika tamthiliya hiyo”,
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF