Leo May 26, 2021 Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amesimama kizimbani na kukana mashtaka 18 yanayomkabili.
Katika kesi ya msingi iliyosikilizwa mahakamani Jijini Pietermaritzburg, mwanasiasa huyo anakabiliwa na tuhuma za rushwa, ukwepaji kodi na utakatishaji fedha.
Akizungumza kwa upole, huku watu wanaomuunga mkono wakiwa wamekusanyika nje ya mahakama, Zuma mwenye umri wa miaka 79 amesema kesi zake ni matokeo ya siasa chafu dhidi yake.
Akifafanua hilo, Zuma hakuwataja majina lakini alisema maadui zake wanatoka ndani na nje ya Chama tawala, African National Congress (ANC).