Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini imetupilia mbali ombi la “haraka” la Rais wa zamani Jacob Zuma la kutaka kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Ijumaa.
Zuma, ambaye ni kiongozi wa chama cha uMkhonto weSizwe (MK), alidaiwa kuwa na kasoro za kura katika uchaguzi wa bunge wa Mei 29.
MK, ambayo iliambulia viti 58 vya ubunge, ilishika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo, nyuma ya chama tawala cha African National Congress (ANC) na chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA).
Siku ya Jumatano jioni, mahakama kuu ya Afrika Kusini iliamua kwamba ombi la chama cha MK lilikuwa ni dharura ya “iliyojitengenezea” na haina mashiko.