NI July 17, 2022 ambapo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ameshiriki katika vikao vya mkutano wa 10 wa Bunge la Kimataifa linalosimamia masuala ya Uvumilivu na Amani unaoendelea katika Bunge la Morocco jijini Rabat.
Mbali na Zungu, wawakilishi wengine kutoka Tanzania kwenye Bunge la IPU ni Esther Matiko, Mwanaisha Ulenge, Ramadhan Suleiman Ramadhan, Joseph Mhagama na Elibarick Kingu.