Zuri Marley, mjukuu wa marehemu nguli wa muziki wa reggae wa Jamaika Bob Marley, amesema mwimbaji wa Nigeria Burna Boy aliyeshinda Grammy ndiye msanii pekee ambaye angemthamini sana kuona kazi yake pamoja na babu yake bob.
Alibainisha hayo alipokuwa akizungumza katika onyesho la kwanza la filamu ya ‘Bob Marley: One Love’ huko London hivi karibuni nakusema alifikiria juu yake vizuri na akashawishika kuwa Burna Boy ndiye msanii pekee ambaye ushirikiano wake na babu yake angependa kuona.
Miss Marley alisema: “Mtu ambaye ningetaka babu yangu [Bob Marley] ashirikiane naye ni Burna Boy. Ilibidi nifikirie juu yake. Nilirudi backstage na niliona kama, ‘Burna Boy-Africa unite.”