Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC ambaye pia ni muwekezaji wa club hiyo Mohammed Dewji leo alikutana na waandishi wa habari na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya timu yao, MO Dewji amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya Simba SC kufungwa magoli 5-0 katika michezo miwili mfululizo.
MO Dewji amewataka watanzania na wana-Simba waiunge mkono timu yao kwani, wanatakiwa kufahamu kuwa Simba imekutana na timu zenye nguvu zaidi yao lakini hiyo haiwakatishi tamaa ya kusema kuwa timu yao haiwezi kufanya chochote katika michuano ya CAF Champions League.
Hata hivyo MO Dewji ameeleza kuwa club kama Al Ahly amesikia hivi karibuni imesajili mchezaji mmoja tu kwa kiasi cha zaidi ya Tsh Bilioni 10, hiyo ikiwa ni mara tano na zaidi ya bajeti ya usajili wa Simba SC, hiyo haiwezi kuwakatisha tamaa Simba SC kujipanga zaidi na kufanya vizuri.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF