Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Saudi Arabia Mfalme Salman ametoa idhini ya wanawake kuendesha magari jambo ambalo halijawahi kutokea nchini humo.
Mfalme huyo amefikia uamuzi huo kutokana na harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza wanawake waruhusiwe kuendesha magari.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Abdallah al-Mouallimi ametangaza habari hizi kwenye mkutano mkuu wa umoja huo jana September 26, 2017 huko New York Marekani. Kwa muda mrefu Saudi Arabia imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari.
Ulipitwa na hii? “Hamuwezi kujua mateso ninayoyapata, ni shida kuwa Rais” – President Magufuli