“Hii vita ni kubwa na tunaenda vitani, kuna watu hapa watapata msukosuko, wenyewe wanajijua, tunachokitaka sisi ni Airtel yetu, hatukuwa na haja sisi kuanzisha simu za mkono kama tungekuwa na Airtel yetu,” ni maneno ya Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Omar Rashid Nundu mbele ya waandishi wa habari leo.
Omar Nundu ameongea hayo ikiwa ni siku moja imepita baada ya President Magufuli kumuagiza Waziri wa Fedha na Mipango kufuatilia suala la Airtel kumilikiwa na TTCL kwa taarifa alizonazo kulifanyika mchezo wa ovyo.
Mwenyekiti huyo wa Bodi amesema wao wanaitaka Airtel yao na kusema wao kama TTCL hawatafuti mgao na wao hawana Hisa katika Airtel zilipo ni za seriakli na mwekezaji, nakutaka Watanzania wajue kwamba Airtel iliyopo kuna kila uhalali kuwa ni kampuni ya TTCL.
HISTORIA: NINI KILIFANYIKA KWA AIRTEL, UHUSIANO WAKE NA TTCL UKO VIPI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA