Stori za Magazeti mengi ya Tanzania yamekua yakijaribu kuwahusisha Mheshimiwa Zitto Kabwe kutoka chama cha ACT na Mheshimiwa Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa kwa sasa hawako kwenye maelewano mazuri yaani hawapatani.
Kwenye Exclusive na millardayo.com, #AyoTv na #Amplifaya Mheshimiwa Zitto Kabwe amekubali kujibu swali hili>>’Mbowe ni kaka yangu amenifata Chuo Kikuu kuja kumsaidia kuijenga Chadema,Nilienda kumsaidia kujenga Chadema tumejenga Chadema pamoja‘
Sentensi nyingine amesema>>’Tumetofautiana katika masuala ya kiuongozi,tumetofautiana kwenye masuala ya kiitikadi,tumetofautiana kwenye masuala ya muono huko tunakokwenda lakini naamini bado ni kaka yangu‘>> Zitto Kabwe.
Mengine unaweza kusikiliza mtu wangu kwa kubonyeza play hapo chini.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.