Usiku wa February 23, 2018 Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro baada ya kukosa dhamana.
Kiongozi huyo anashikiliwa tangu Saa 3: 30 usiku wa leo alipokamatwa kwa kufanya mkusanyiko bila kibali. Zitto alikamatwa katika Kata ya Kikeo iliyopo wilayani Mvomero na alitarajiwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dakawa lakini akahamishiwa Morogoro Mjini.
Wakili wa Zitto Kabwe, Emmanuel Lazarus Mvula amesema licha ya Zitto kukamilisha kuandika maelezo ila bado wamezuia dhamana ya mteja wake wakisubiri maelekezo.
” Jeshi la Polisi limekataa kusema kama dhamana ipo wazi ama la, na kama ipo wazi masharti yake ni yapi, na wamekataa pia kusema iwapo leo watampeleka mahakamani kwa mujibu wa sheria au la,” -Mvula.
BREAKING: WATU 28 WALIOKAMATWA ‘SIKU YA KIFO CHA AKWILINA’ WAPANDISHWA KIZIMBANI