Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, February 11, 2018 alimtembelea Mbunge Singida Mashariki Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji.
Zitto amesema amefurahi kumwona Lissu akiwa anaendelea vizuri, na afya yake kuzidi kuimarika. Akilinganisha na hali aliyomwona nayo jijini Nairobi mwaka 2017, amekiri kuwa Mwenyezi Mungu amepitisha uwezo wake na kumponya Lissu.
Zitto ametaja baadhi ya mambo ambayo amezungumza na Lissu ambayo yanahusu Tanzania na pia kuhusu suala la matibabu yake
“Lissu anasikitika kuwa Bunge mpaka leo sio tu halimhudumii lakini hata stahili zake za msingi kama Mbunge hapewi. Licha ya kutibiwa kwa misaada ya wasamaria wema, lakini ana mahitaji mengine kama mwanadam na wajibu kama mzazi. Sheria ya Bunge imeweka wazi kuwa Mbunge anapokuwa ametibiwa nje ya nchi Bunge humgharamia maisha yake.” -Zitto Kabwe
“Mpaka sasa ni miezi mitano imepita tangu Lissu ashambuliwe kwa risasi na hakuna taarifa yeyote kuwa mamlaka za uchunguzi zimewakamata wahusika au kuonyesha tu juhudi za kuwatafuta wahusika. Jambo hili linatoa taswira mbaya sana juu ya vyombo vyetu vya uchunguzi, linajenga chuki na linaondoa imani ya wananchi kwa vyombo hivyo.” Zitto Kabwe
Wafanyakazi 800 wapunguzwa kazini, Mkurugenzi atuma ombi kwa JPM