Top Stories

Mwigulu amemuona Rais Magufuli akipokea ndege mpya ameandika haya

on

Leo July 8, 2018 Rais Dr. John Pombe Magufuli ameipokea ndege mpya aina Boeing 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini DSM.

Baada ya mapokezi hayo baadhi ya watu wamekua wakitoa pongezi zao ambapo hapa nakusogezea alichoandika aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ambapo ameandika katika ukurasa wake Twitter.

Nanukuu “Historia nyingine imeandikwa, tunakila sababu ya kujivunia maendeleo haya, Asante serikali yetu chini ya Rais J.Magufuli kwa hatua hii nyingine kubwa ya kuipeleka nchi yetu mbele katika usafiri wa anga.”

BREAKING: JPM AKIPOKEA NDEGE MPYA YA ATCL AIRPORT – DSM

Soma na hizi

Tupia Comments