Tangaza Hapa Ad

Mix

Ombi la Meck Sadiq kuhusu mkoa wake wa Kilimanjaro

on

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiq ameiomba taasisi ya GSM Foundation kurudi tena mkoa huo na kuendesha kambi tiba nyingine ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ili kutimiza lengo la kutibu watoto zaidi ya 50 walioko vijijini ambao wamechelewa kufikiwa na taarifa ya kambi hiyo.

Ombi hilo amelitoa mbele ya Kaimu mkuu wa kambi tiba ya GSM Dk Lemeri Mchmoe kutoka Taasisi ya  Mifupa na upasuaji ya Muhimbili MOI,  wakati mkuu huyo wa mkoa alipokuwa akikagua maendeleo ya watoto waliofanyiwa upasuaji katka hospitali ya KCMC iliyopo jijini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

3-2

Meck Sadiq amesema wagonjwa wengi wenye changamoto za tiba wako vijijini na huwachukua siku kadhaa kufika hospitalini hivyo inawezekana wakachelewa kufika kwa wakati kutibiwana kambi tiba hiyo inayodhaminiwa kwa asilimia mia moja na GSM Foundation.

Mpaka sasa kambi tiba ya GSM Foundation imeshabitia zaidi ya watoto 150 na kuwaona watoto zaidi ya 1000  na imepita katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Singida, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Songea, Mbeya na Iringa.

2-2

Mikoa mingine ambayo imeshafaidika na kambi tiba ya GSM Foundation ni Pwani na Tanga, na sasa kambi iko Mkoani Kilimanjaro ikiendelea na ziara zake ambapo inaelekea Arusha na Mara.

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV, SEPTEMBER 22 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement