Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kauli ya Guardiola baada ya Nasri kusema walikatazwa wasifanye mapenzi

on

Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Sevilla ya Hispania kwa mkopo akitokea Man City Samir Nasri siku kadhaa nyuma alisikika akisema ocha wa Man City Pep Guardiola aliwakataza wachezaji wasifanye mapenzi baada ya saa sita usiku ili wapate muda wa kutosha kupumzika.

Stori kutoka BBC Sport akinukuliwa kocha wa Man City Pep Guardiola akizungumzia ishu hiyo, ameeleza kuwa hajawahi kukataza wachezaji kufanya mapenzi na wapenzi wao na anaamini kuwa mchezaji akifanya mapenzi ndio anacheza vizuri.

37a8d10500000578-0-image-a-1_1472462703090

Nasri na Pep Guardiola

“Haiwezekani kuwa mchezaji mzuri kama hufanyi mapenzi na mpenzi wako, sijawahi kukataza wachezaji wasifanye mapenzi na sitakataza kama utakuwa ukifanya hivyo wewe ni mchezaji mzuri” >>> Guardiola

Hata hivyo Pep Guardiola amewahi kuripotiwa kuweka sheria kadhaa katika kikosi chake cha Man City ili kujenga timu yenye mshikamano, Guardiola anaripotiwa kupiga marufuku huduma za Wi-fi katika maeneo ya uwanja wa mazoezi ya Man City.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement