Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Magoli ya mechi za Leicester vs Man United, Man City vs Swansea na msimamo wa EPL ulivyo

on

Baada ya Jumamosi ya February 4 2017 kuchezwa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017, Jumapili ya February 5 ilichezwa michezo miwili ya Ligi Kuu England, Leicester City walicheza dhidi ya Man United na Man City dhidi ya Swansea City.

Michezo hiyo ilimalizika kwa Man United kupata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Leicester, magoli yakifungwa na Makhitaryan dakika ya 42, Zlatan Ibrahimovic dakika ya 44 na Juan Mata dakika ya 49, ushindi huo umeifanya Man United kuendelea kuwepo nafasi ya 6 katika msimamo wa EPL.

Wakati Man City wakiwa katika uwanja wao wa Etihad wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Swansea City, magoli yakifungwa na mchezaji wao wa kibrazil Gabriel Jesus dakika ya 11 na 90 huku goli la Swansea likifungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 81.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement