Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Mix

BREAKING: Ujumbe wa Masoud Kipanya uliothibitisha kupatikana kwake

on

Baada ya kuenea kwa taarifa zilizowashitua wengi leo January 1 2018 kuhusiana na mtangazaji wa Clouds FM na mchoraji katuni mahiri Masoud Kipanya kudaiwa kupotea.

Muda mchache baada ya uongozi wa Clouds Media Group ambao ndio waajiri wa Masoud Kipanya kutoa taarifa na kuomba watu wawe watulivu itatoa taarifa rasmi kuhusiana na habari hizo.

Kupitia ukurasa rasmi wa instagram wa Masoud Kipanya umetoa taarifa inayoashiria kuwa Masoud Kipanya amepatikana na yupo salama ila imeeleza kuwa kuenezwa kwa taarifa za kupotea kwake katika mitandao ya kijamii kumesaidia kupatikana kwake.

Taarifa ya instagram ya Masoud Kipanya inaeleza hivi “Poleni kwa usumbufu na asanteni kwa kujali hali za wengine, niko salama Alhamdulillah. Namshukuru pia aliyesambaza taarifa ‘AMESAIDIA’

A post shared by Masoud Kipanya (@masoudkipanya) on

Taarifa ya Clouds Media Group kuhusu Masoud Kipanya kupotea

Soma na hizi

Tupia Comments