Tangaza Hapa Ad

Michezo

Pesa aliyoitoa Messi kwa familia za wachezaji waliofia katika ajali ya ndege

on

Bado dunia na ulimwengu wa soka kwa ujumla unaomboleza msiba wa msafara wa timu ya Chapocoense ya Brazil uliyopata ajali ya ndege wakati wakielekea kutua uwanja wa ndege wa Medellin Colombia, kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa kwanza wa fainali ya Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia.

Ajali hiyo ya ndege imesababisha vifo vya watu 76 kati ya 81 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo huku watu 72 wakitajwa kuwa ni msafara wa timu hiyo, mshambuliaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina ambaye pia anatokea bara la America Kusini Lionel Messi ameguswa na msiba huo.

screen-shot-2016-11-30-at-1-35-19-pm

Kupitia mtandao wa fcbarca.me umeripoti kuwa Lionel Messi ameamua kutoa euro milioni 5.3 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 12.2 kwa timu ya  Chapecoensea na familia za wachezaji wa timu hiyo, Lionel Messi anaungana na staa mwenzake Cristiano Ronaldo ambaye ametoa zaidi ya Tsh bilioni 6.9.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement