Tangaza Hapa Ad

Michezo

Msimamo wa Simba ili wakubali kucheza mzunguko wa pili wa VPL na Yanga

on

Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba leo November 23 2016 kupitia kwa afisa habari wao Haji Manara wameweka wazi msimamo wao kuwa hawatokuwa radhi kucheza dhidi ya watani zao wa jadi Yanga mzunguuko wa pili kama waamuzi hawatotoka nje ya nchi.

Maamuzi hayo ya Simba yanakuja ikiwa zimepita wiki kadhaa toka wacheze na watani zao wa jadi Yanga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Kufuatia mchezo huo ambao katikati ya mchezo mashabiki wanaoaminika kuwa wa Simba walivunja vitu kutokana na goli la Yanga lililofungwa na Amissi Tambwe, alifunga akiwa kasogeza mpira kwa mkono kabla ya kufunga na refa Martin Saanya akalikubali goli licha ya mpira kusimama kwa dakika kadhaa.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement