Tangaza Hapa Ad

Michezo

Abdi Banda wa Simba amefungiwa

on

Beki wa timu ya Simba SC Abdi Banda amekutana na adhabu ya kufungiwa michezo miwili na kamati ya haki na hadhi za wachezaji baada ya kukutwa na kosa la kumpiga mchezaji wa Kagera Sugar wakati wa mchezo dhidi ya Simba dhidi ya Kagera.

Banda alifanya kosa hilo wakati wa mchezo huo uliyochezwa April 2 2017 katika uwanja wa Kaitaba Bukoba kwa kumpiga ngumi George Kavilla wa Kagera Sugar lakini adhabu yake imepungua kutokana na Banda kuwa alimuomba radhi Kavilla lakini pia alikiri kosa.

Abdi Banda

Sasa Banda ana nafasi ya kuendelea kuitumikia Simba katika michezo mitatu iliyosalia baada ya kumaliza kuitumikia adhabu hiyo, katika mchezo huo Simba ilifungwa na Kagera kwa magoli 2-1, taarifa za Banda kufungiwa zimetolewa na mtandao wa salehjembe.com

VIDEO: Game haikuoneshwa Yanga vs MC Alger, nimeyanasa matukio na goli la Yanga FT 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement