Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA 10: Waziri Nchemba alivyowapatia ushindi wabunge wa Yanga vs Simba

on

Septemba 25 2016 ilikuwa ni siku ambayo wabunge wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walicheza mchezo wa hisani kwa ajili  ya kukusanya fedha za watu waliopata na tetemeko la maafa Bukoba, wabunge walijigawa katika timu mbili wale wabunge ambao wanaishangilia Yanga na wabunge wa Simba.

img-20160925-wa0014

Mashabiki ambao walikuwa wamejitokeza uwanjani kuangalia wabunge hao wakiwa katika mavazi ya timu wanazozishabikiwa mbunge na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba alikuwa ni miongoni mwa wabunge waliowanyanyasa wabunge wa Simba kwa kuwaonesha uwezo mkubwa katika kuuchezea na kumiliki mpira.

img-20160925-wa0013

Hata hivyo katika mchezo huo ambao waziri Mwigulu aliifungia magoli mawili timu ya timu ya wabunge wa Yanga kati ya ushindi wa goli 5-2, waziri Mwigulu alionekana kuwasumbua baadhi ya wabunge kwa kupiga chenga, hadi dakika 90 zinamalizika wabunge wa Yanga waliondoka na ushindi wa goli 5-2.

img-20160925-wa0016

Magoli ya wabunge wa Yanga yalifungwa na Jadal Hamisi dakika ya 4, Musa Sima dakika ya 5, Hamidu Bolali dakika ya 9 na mwisho Mwigulu Nchemba akahitimisha kwa kufunga magoli mawili ya mwisho na kuwafanya wabunge wa Yanga kuondoka na Kombe la Ubingwa wa mchezo huo wa Hisani.

img-20160925-wa0015

img-20160925-wa0012

img-20160925-wa0011

img-20160925-wa0079

img-20160925-wa0010

img-20160925-wa0009

img-20160925-wa0008

img-20160925-wa0020

GOALS: TP Mazembe vs Yanga August 23 2016, Full Time 3-1 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement