Michezo

Jezi maalum atakayoivaa Samatta yenye ‘Golden Bull’ mgongoni

on

Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji leo Jumamosi ya November 3 2018 ataingia uwanjani kucheza game yao ya 14 dhidi ya Club Brugge katika uwanja wa Luminus Arena.

KRC Genk watakuwa nyumbani na tayari ikiwa siku moja kabla ya mchezo huo tiketi zote zimeripotiwa kuuzwa, hivyo ka mashabiki ambao hawana tiketi wasitegemee kwa siku ya Jumamosi ya November 3 wataweza kuzipata.

Kingine cha kufahamu ni kuwa Samatta katika mchezo huo atavaa jezi maalum yenye ‘Golden Bull’ mgongoni kutokana yeye ndio mchezaji wa KRC Genk mwenye magoli mengi baada ya kumpiku Leandro Trossard aliyekuwa na magoli nane na sasa Samatta amefunga magoli 10 Ligi Kuu.

Game ya Genk dhidi ya Club Brugge inamvuto mkubwa katika Ligi hiyo kutokana wanakutana timu zinazofuatana katika Ligi Kuu Ubelgiji, KRC Genk wakiongoza Ligi hiyo yenye timu 16 kwa point 33 wakati Brugge wakiwa nafasi ya pili wakiwa na point 30.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments