PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

Kiongozi wa Mbio za Mwenge alivyogoma kuzindua Zahanati mbele ya DC Ally Hapi

on

Leo July 9, 2018 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni DSM, Ally Hapi amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Wilaya ya Kigamboni na kushiriki uzinduzi wa miradi mbalimbali ndani ya Wilaya yake.

Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho amegoma kuzindua jengo la Zahanati ya Mkoroshini iliopo Msasani kutokana na gharama zilizotajwa kutumika kwa ujenzi wa jengo hilo kuwa Milioni 406 ambazo haziendani na kiwango cha jengo hilo.

Kabeho amewataka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuingilia kati suala hilo kwa undani ili kuweza kubaini wizi uliofanyika katika jengo hilo.

“Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 haujaridhika na gharama za ujenzi wa jengo hili hivyo sitaweka jiwe la msingi, taratibu zote zikifanyika nikajiridhisha nitaweka jiwe la msingi kwa utaratibu” amesema Kabeho

Tume anayoitaka Mke wa Bilionea Erasto Msuya iundwe

 

Soma na hizi

Tupia Comments