Tangaza Hapa Ad

Michezo

Bravo kaweka wazi kilichomfanya aondoke FC Barcelona

on

Golikipa namba moja wa Manchester City aliyejiunga na klabu hiyo msimu huu akitokea FC Barcelona ya Hispania Claudio Bravo Septemba 19 ameweka wazi kilichomuondoa FC Barcelona na kuamua kujiunga na Man City pamoja na kuweka wazi uhusiano wake na golikipa mwenzake Ter Stegen.

Bravo amezungumza kilichomuondoa FC Barcelona na kuamua kujiunga na Man City, kutokana na kutotaka kusaini mkataba mwingine FC Barcelona halafu aishie kukaa benchi, ni kweli uwepo wa Ter Stegen umemfanya aondoke FC Barcelona lakini sio kweli kama walikuwa na ugomvi na kipa huyo kama ambavyo inadaiwa na baadhi ya watu.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Claudio Bravo alijiunga na Man City katika dirisha kubwa la usajili la majira ya joto mwaka huu 2016 na kurithi nafasi ya Joe Hart ambaye kocha Pep Guardiola aliamua kumtoa kwa mkopo kwenda katika klabu ya Torino ya Italia.

terstegenbravo160804b

Ter Stegen na Bravo wakati wakiwa FC Barcelona pamoja

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement