PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Kyliane Mbappe bado anaendelea kuguswa na ajali ya Emiliano Sala na rubani wake

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa pia Kyliane Mbappe, amezidi kuonesha uungwana kwa familia ya rubani wa Emiliano Sala aliyepata nae ajali wakiwa pamoja katika ndege moja January 21 2019.

Mbappe ambaye pesa zake zilikuwa sehemu ya watu waliochangia kuendesha zoezi la pili la utafutwaji wa ndege iliyokuwa imepotea ikiwa na mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sala akiwa na rubani wake David Ibbotson, leo Mbappe amemua kuongeza tena pesa.

Emiliano Sala na rubani wake David Ibbotson

Pamoja na kuwa zoezi la pili liliendeshwa na kuipata ndege ikiwa chini ya maji na mwili wa Emiliano Sala, familia ya rubani David Ibbotson iliamua jana kutangaza kuchangisha zaidi ya pound 300000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 800, kwa ajili ya kuendelea kuutafuta mwili wa rubani huo ambao haujaonekana hadi leo hii, Mbappe ameamua kuchangia tena kiasi cha pound 27000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 80 kwa ajili ya kuiwezesha familia ya David Ibbotson iendeshe zoezi la kumtafuta rubani huyo.

“Tunashindana na timu zenye nguvu, aliyetoa assist Alexandria kanunuliwa Bilioni 10”-MO Dewji

Soma na hizi

Tupia Comments