Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mchezaji wa Chapecoense Alan Raschel ametaja mchezaji mwenzake alivyomuokoa katika ajali ya ndege

on

Beki wa Chapecoense ya Brazil Alan Raschel aliyenusurika katika ajali ya ndege November 29 2016  Colombia walipokuwa wanaelekea kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Club Bingwa America Kusini dhidi ya Atletico Nacional, ameonekana uwanjani kwa mara ya kwanza.

Raschel ni miongoni mwa watu sita walionusurika katika ajali iliyoua watu 71 wakiwemo na waandishi wa habari, December 22 2016 Raschel alihojiwa na kituo cha TV cha Brazil na kueleza kuwa mchezaji mwenzake Jackson Follman alisaidia kunusuru maisha yake.

resizer

Jackson Follman

“Kabla ya kuanza safari Jackson Follman aliniomba nibadili siti na kukaa nae pamoja na mimi nilimsikiliza, kwa heshima yake kwa sababu nimefahamiana na Follman toka 2007, nikahama pale na kwenda kukaa nae kumbe kufanya vile kulisaidia kuokoa maisha yangu kutoka nilipokuwa nimekaa”

Jackson Follman ambaye ni golikipa wa Chapecoense ni miongoni mwa watu 6 waliyonusurika katika ajali, lakini imeripotiwa kuwa hatoweza kurudi uwanjani na kucheza soka kutokana na kuumia mguu na kupelekea kukatwa, lakini Chapecoense imemuahidi kumpa kazi katika kipindi chote cha maisha yake.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement