Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Keki iliyodumu zaidi ya miaka 100 bila kuharibika, imegunduliwa Antarctica

on

DUNIA hakika haiishiwi na mambo – na kila jambo lina namna yake ya kutokea liwe limesimuliwa au limeandikwa. Moja ya mambo ambayo yamekuwa gumzo kwa sasa ni hii Keki ambayo imegunduliwa katika moja ya majengo ya zamani huko Antarctica ikisemekana kuhifadhiwa kwa miaka zaidi ya 100.

Keki hiyo ambayo ilitengenezwa na Kampuni ya zamani ya kutengeneza Biscuit ya Uingereza Huntley & Palmers, licha ya kukaa kwa muda huo lakini inasemekana kuwa haijaharibika ingawa chombo kilichotumika kuhifadhia kimeharibika kwa kutu.

Keki hiyo ilikutwa kwenye shelfu ndani ya kibanda Cape Adare kilichotumika na Northern Party mwaka 1911, ambapo watafiti wanadai iliachwa hapo na inaaminika ilikuwa mali ya Northern Party, na kwa mujibu wa nyaraka zilizokutwa ni kwamba ilichukuliwa katika Maonesho ya Terra Nova kati ya 1910 na 1913.

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement