Michezo

Yanga mambo magumu vs Rayorn Sports uwanja wa Taifa

on

Jumatano ya May 16 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam Yanga walikuwa wenyeji wa Rayon Sports ya Rwanda kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi D wa kombe la shirikisho Afrika CAF.

Yanga wakiwa nyumbani wameshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kujikuta wanalazimishwa sare tasa (0-0) hivyo wanakuwa na point moja na wakishika mkia katika Kundi D ambalo linaongozwa na USM Alger ambayr ana point nne.

Kwa upande wa game ya USM Alger dhidi ya Gor Mahia waliyopo Kundi moja na Yanga, mchezo wao umemalizika kwa sare tasa pia hivyo Gor Mahia na Rayon Sports wote wanabaki kuwa na point mbili mbili kila mmoja, Yanga sasa atahitaji kuutumia vizuri mchezo wake wa tatu dhidi ya Gor Mahia kama atakuwa ameweka dhamira ya kweli ya kusonga mbele michuano ya CAF.

Haji Manara alivyokuja na takwimu leo mbele ya waandishi wa habari

Soma na hizi

Tupia Comments