Biko


Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi

on

Rais John Magufuli leo December 6, 2017 amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi 6 za taasisi za Serikali baada ya wenyeviti waliokuwepo kumaliza muda wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Rais amemteua Monica Ngenzi Mbega kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko huku Prof. Egid Beatus Mubofu akiwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC).

Pia amemteua Prof. Abiud Kaswamila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Prof. Esther Hellen kushika Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Dkt. Kenneth akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi ya kifedha ya Self Microfinance Fund Limited pamoja na Dr. Titus Mlengeya Dismas Kamani kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania.

Ulipitwa na hii?Tume ya Taifa ya Uchaguzi yafunguka kuhusu uchaguzi wa madiwani

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement