Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu

on

Leo February 14, 2018 nakusogezea stori inayomhusu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kama chambo ya kisiasa katika majukwaa.

Dr. Mwigulu aliyasema hayo February 13, 2018 mkoani Singida wakati wa kampeni za udiwani katika kata ya Mitunduluni. Amewataka waache kutumia matatizo ya ndugu yao kama mitaji ya kisiasa baadala yake waje na hoja za maana za kusaidia katika maendeleo ya nchi.

Aliongeza kusema kuwa mwaka uliopita uhalifu wa ajabu ulitokea ambapo kuna watoto wadogo wa chekechea walitekwa na kuuwawa na wazazi wao ni watu wa kawaida kabisa na kuhoji kama serikali pia imehusika kwenye hilo.

“Sisi tunaoshughulika na maswala ya uhalifu tunatafuta wahalifu wanaofanya maswala ya kihalifu, kuna watu wanaona ni agenda ya kisiasa wakati sisi tuombea mtu apone.”-Dr. Mwigulu

Dr. Mwigulu ameongeza kwa kusema kuwa je angeamua kuendelea kusema kuhusu kupigwa risasi kwa mwanajeshi masaki ina uhusiano gani na shida za kata ya mitundulini, hivyo wananchi wa Singida wawaadhibu kwa kuwanyima kura katika uchaguzi wa tarehe 17 mwezi huu.

BREAKING: Kamanda Kinondoni Kuhusu Mwili Uliokotwa Coco Beach

Baada ya Wizara ya AFYA kuhamia Dodoma, Jengo lao wamepewa wengine?

 
 

Soma na hizi

Tupia Comments