Tangaza Hapa Ad

fB insta twitter

Unaambiwa hivi ndivyo ‘Chips dume’ zinavyoweza kuwa chanzo cha kisukari

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya yaliyondikwa kwenye gazeti la Nipashe ni ripoti ya utafiti huu wenye kichwa cha habari ‘Chips dume zinavyoweza kuwa chanzo cha sukari

Gazeti la Nipshe limeripoti kuwa pengine hii ni taarifa ya kushtua kuhusiana na masuala ya afya, hasa kwa wakazi wa mijini. Ni kwamba mihogo ya kukaanga maarufu kama ‘chips dume’ ni miongoni mwa vyakula vilivyobainika kuwa vinaweza kuwa chanzo cha aina mojawapo ya maradhi ya kisukri (type 2 diabetes).

Aidha, mbali na chips dume, vyakula vingine vyote vinavyokaangwa kwa mafuta vinaweza kuwa chanzo cha maradhi hayo ya kisukari endapo uandaaji wake hautafanyika kwa kuzingatia tahadhari za kiafya.

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliyotolewa hivi karibuni, ni kwamba vyakula vilivyoandaliwa kwa kuchemshwa au kuivishwa kwa mvuke ndiyo pekee vilivyo salama zaidi kwa sababu ya kutokuwa na tishio hilo la kisukari kwa walaji, wakati mihogo, viazi na vyakula vingine vinapokaangwa au kuokwa au kuchomwa hutoa kemikali iitwayo glycation.

Aidha, kunapokuwa na kiwango cha juu cha kemikali hiyo, matokeo yake huwa kunatokea ukinzani dhidi ya insulin kwa mlaji wa chakula husika na matokeo yake ni uwezekano wa maradhi ya kisukari kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo.

Kwa kawaida insulin ni aina ya kichocheo (homoni) ndani ya mwili ambacho husaidia kurekebisha kiwango cha sukari ambacho ni chanzo cha nishati mwilini. Bila ya kuwa na insulin au kukiwa na ukinzani dhidi ya insulini, kiwango kikubwa cha sukari hubaki kwenye damu. Hali hiyo pia inaweza kusababisha matatizo ya moyo, macho, figo, na ogani nyingine mwilini.

Unaweza kupitia habri nyingine zilizoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania September 18 2016

ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUPOKEA MSAADA KUTOKA KENYA NA UGANDA KWA JILI YA MAAFA YA KAGERA? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement