Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA 7: Goli la kwanza la Coutinho laipeleka Barca fainali

on

Staa mpya wa Klabu ya Barcelona aliyetoka Liverpool Philippe Coutinho ameisaidia Klabu yake mpya ya Barcelona kutinga fainali ya Kombe la Mfalme  (Copa del Rey) kwa kuifunga klabu ya Valencia goli 2-0 usiku wa kuamkia leo February 9, 2018.

Magoli ya Barcelona yamefungwa na Ivan Rakitic na mshambuliaji mpya Philippe Coutinho ikiwa ni goli lake la kwanza tangu ajiunge klabuni hapo..

Barcelona wamefanikiwa kufuzu kwa  magoli 3-0 baada ya mchezo wa kwanza Barcelona kushinda goli 1-0 na sasa Klabu hiyo itakutana na Sevilla kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme itakayochezwa April 21, 2018.

MANARA AMEWAOMBA MASHABIKI WA SIMBA WAKAISHANGILIE YANGA

 

Soma na hizi

Tupia Comments