Tangaza Hapa Ad

fB insta twitter

Kijana Singida anyofolewa ulimi na mke wa jirani yake wakati ‘wakikiss’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti September 16 2016 ni hii kutoka gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Anyofolewa ulimi’

Kijana mkazi wa Unyakhae nje kidogo ya mji wa Singida, Said Mnyambi (26) amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kunyofolewa kipande cha ulimi wake na mke wa jirani yake aliyekuwa anamlazimisha kufanya nae mapenzi.

Kwa mujibu ya maelezo ya kijana huyo, tukio hilo limetokea siku ya Idd El Haji Jumatatu wiki hii saa 3:30 usiiku.Alieleza kuwa siku ya tukio, mke wa jirani yao mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake, alimwomba amsindikize nyumbani kwa kuwa amelewa .

Alidai walipofika njiani,mama huyo alimtaka wafanye naye mapenzi jambo ambalo kijana huyo alimkatalia lakini alimwomba angalau waagane kwa kunyonyana ulimi (denda) naye akamkubalia.

Nilimkubalia kumpa denda na hapo ndipo alipoanza kufungua mkanda wa suruali yangu, lakini nilipomkatalia kufungua mkanda wangu hapo ndipo alipong’ang’ania ulimi wangu hadi akanyofoa kipande na yeye akakimbilia kwake’;- Said Mnyambi

Alipoulizwa iwapo mama huyo ni mpenzi wake, kijana huyo alikataa kata kata na kujitetea kuwa alimuomba amsindikize kwa vile tu anamfahamu na ni jirani yake.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dk Ramadhani Kabala alithibisha kunyofolewa kwa kipande cha ulimi wa kijana huyo na kueleza kuwa alifika hospitalini hapo kwa matibabu baada ya ulimi wake kupata maambukizi na kuingia usaha hadi kushindwa kuongea.

Unaweza kupitia habari zingine kwenye magazeti ya Tanzania

ILIKOSA HII YA MTANZANIA ANAYEFANYA KAZI TAASISI YA BILL GATE, ALIWAHI KUWA WA MWISHO DARASANI? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement