Michezo

Europa League KRC Genk na Arsenal sare nyumbani, Welbeck atolewa na machela

on

Usiku wa November 8 2018 michezo ya UEFA Europa League hatua ya makundi round ya nne msimu wa 2017/2018 iliendelea tena kwa michezo kadhaa kuchezwa, KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta walikuwa nyumbani kuwakaribisha Besiktas ya Uturuki wakati Arsenal wao walikuwa London katika uwanja wao wa Emirates kuisubiri Sporting CP ya Ureno.

KRC Genk wakiwa nyumbani wameendelea kuongoza Kundi lao I kwa kutoka sare ya 1-1 na Besiktas, magoli yakifungwa na Ricardo Quaresma dakika ya 16 upande wa Besiktas, wakati upande wa KRC Genk lilifungwa na Sander Berge dakika ya 88 na mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Sare hiyo bado inawafanya KRC Genk kuendelea kutawala kilele mwa msimamo wa Kundi I baada ya kufikisha point saba, huku Besiktas wao wakiwa nafasi ya mwisho kwa kuwa na point nne, wakati Sarpsborg 08 wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point tano sawa na Malmo ya Sweden walipo nafasi ya tatu.

Kwa upande wa Arsenal wao walijikuta wakiondoka uwanjani wakiwa sare tasa 0-0 lakini ni pigo kwao kwa mchezaji wao Danny Welbecki kushindwa kumaliza mchezo na kuishia dakika ya 27 baada ya kuumia vibaya, Arsenal wanaongoza Kundi E kwa kufikisha jumla ya point 10, wakifuatiwa na Sporting CP wenye point saba na kuwaacha Vorskla Poltava na Qarab wakibaki na point tatu kila mmoja.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments