Michezo

Haya ni maamuzi ya Steve Gerrard baada ya msimu huu wa Ligi kuisha…

on

245E330A00000578-2893769-image-m-33_1420152144267Nahodha huyo wa zamani wa England, Steven Gerrard anamaliza mkataba wake na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na amechukua uamuzi wa kutoongeza mkataba mpya.

Liverpool walimpa ofa mpya Gerrard mwezi November mwaka jana lakini kiungo huyo mwenye miaka 34 alifikia uamuzi wa kutaka kwenda sehemu nyingine kupata changamoto mpya.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na klabu ya Liverpool Steven Gerrard amesema;”Nimeamua kutangaza uamuzi huu sasa ili kocha na timu isipoteze umakini kwenye mambo ya msingi kutokana na tetesi juu ya hatma yangu.

Liverpool Football Club ni sehemu kubwa ya maisha yangu na jambo hili la kuondoka hapa ni uamuzi mgumu zaidi niliowahi kufanya katika maisha yangu, lakini ni uamuzi ambao utakuwa na faida kwa watu wote wanaohusika, ikiwemo familia yangu na klabu yenyewe.”– Gerrard.

Nitaendelea kucheza soka lakini siwezi kuthibitisha wapi nitaenda baada ya kutoka hapa, ila kwa uhakika kabisa haitokuwa hapa nikimaanisha sitoichezea klabu ambayo itakuwa na upinzani au itacheza dhidi ya Liverpool – hilo ni jambo ambalo nawaahidi mashabikiwa Liverpool.” — Gerrard.

Gerrard alianza rasmi kuitumikia Liverpool mwaka 1998, mpaka sasa anatajwa kuwa mmoja ya wachezaji bora kabisa wa muda wote wa klabu hiyo akiwa ameichezea mechi 695  na kufunga magoli 177.

Haya hapa ni makombe ambayo amewahi kutwaa akiwa na Liverpool.

Champions League -2 

FA Cups- 2

League Cups- 2 

UEFA Cup- 2

UEFA Super Cups- 2

Charity Shield- 2

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments