Michezo

Tukio la refa kupigwa kichwa? Haji Manara hajalifumbia macho

on

Moja kati ya matukio yaliochukua headlines kwenye soka ni pamoja na hili la beki wa kati wa club ya Yanga SC kudaiwa kumpiga kichwa muamuzi wa mechi kati ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons iliyochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya kumalizika kwa Yanga kupata ushindi wa magoli 3-1.

Mchezo huo ulitawaliwa na presha kubwa kutokana na Yanga kutanguliwa na hatimae kuja kusawazisha na kupata ushindi dakika za lala salama, moja kati ya matukio yaliochukua headlines ni beki wa Yanga Andrew Vincent kudaiwa kumpiga kichwa muamuzi wa game hiyo na pasipo kuoneshwa kadi nyekundu

Kupitia ukurasa wa instagram wa Haji Manara hajaichulia poa na amepaza sauti kwa Bodi ya Ligi kwa kitendo hiko “Ni Tanzania tu muamuzi anapigwa kichwa hadharani kisha hatoi red card, halafu hii ni mara ya ngapi tukio hili linafanyika kwa beki hodari aliyepo timu ya Taifa? Michezo ni uungwana sio vita, bodi ya Ligi Mpo?”>>> Haji Manara

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments