PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Mourinho kakataa kuipa ushirikiano MU TV ya Club yake

on

Kocha Mkuu wa Club ya Man United Jose Mourinho anaripotiwa kuwa atakutana na changamoto mpya katika game ya Man United dhidi ya Arsenal itakayochezwa uwanja wa Old Trafford lakini anatajwa kuwa ana presha ya mashabiki kucheza katika uwanja wa nyumbani.

Arsenal wataingia bila presha sana kutokana na wao kuwa na matokeo mazuri na rekodi nzuri ya kutopoteza katika michezo 19 mfululizo hivi karibuni wakati Man United wao hawana msimu mzuri sasa na wanasuasua kuitafuta TOP 4, hivyo inawezekana Man United wakakutana na wakati mgumu tena kesho

Kuelekea mchezo huo Mourinho alizua kihoja baada ya kukata kujibu swali aliloulizwa na MU TV ambayo ni TV ya Club yake kwa kusema kuwa swali hilo lilitakiwa kuulizwa na muandishi wa kutokea Arsenal TV na sio wa MU TV, kauli ambayo imetafsiriwa kuwa ni kujibu swali lile tena likiulizwa na mtu Man United ni kutoa mbinu za timu kwa wapinzani.

Swali lilikuwa linahusiana na safu ya ulinzi ya Man United itakuwaje kesho, sehemu ambayo inaonekana kuwa na changamoto kubwa kwa Man United msimu huu, Mourinho alipoulizwa alijibu hivi “Sitaki kukujibu wewe nataka  Arsenal TV ndio waulize swali kama hilo niwajibu lakini hawataki, kwa hiyo kwa nini nikujibu wewe” 

Man United wanaingia katika mchezo wa kesho dhidi ya Arsenal wakiwa nafasi ya 7 katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu wa 2018/2019 wakiwa na point 22 wakati Arsenal wapo nafasi ya nne wakiwa na point 30 tofauti ya point nane dhidi ya Man United ambao wamepoteza michezo minne EPL na Arsenal michezo miwili.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments