Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Bei ya dawa ya mafua yamsababishia mwanamke kifo

on

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Heather Holland, 38, ambaye alikuwa mwalimu amefariki Dunia baada ya kushindwa kununua dawa ya mafua kutokana na gharama yake kuwa kubwa nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mume wa marehemu Frank Holland, mkewe alipokwenda hospitali alikuta dawa hizo za mafua ni Dola za Marekani 116 ambayo ni sawa na Tshs 278, 000 hivyo akaamua kuacha kununua jambo lililosababisha kifo chake.

Frank amesema alikwenda kununua dawa hizo siku moja kabla ya kifo cha mkewe ili aanze kuzitumia lakini alikuwa amekwisha chelewa.

Heather ambaye alikuwa mwalimu wa Ikard Elementary School huko Weatherford, Texas ameacha mume na watoto wawili, wakike mwenye miaka 10 na mwingine wakiume mwenye miaka 7.

BOMOABOMOA: Nyumba zilizojengwa karibu na Reli zilivyobomolewa Arusha

Vitu alivyosisitiza IGP Sirro akimuapisha Kamishna wa Zanzibar ‘Polisi tunachangamoto’

 

Soma na hizi

Tupia Comments