Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Mbwana Samatta kamvulia kofia Kelvin Yondani

on

Jumapili ya April 29 2018 mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ulichezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kuhudhuriwa  na mashabiki mbalimbali, dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 1-0 lilifungwa na Erasto  Nyoni dakika ya 38, mchezo huo ulikuwa na presha na matukio mbalimbali yalijitokeza.

Moja kati ya tukio lilijitokeza la Kelvin Yondani kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba kiasi cha kufanya mjadala kuwa mkubwa mtandaoni, watu mbalimbali wameizungumzia ishu hiyo na kutoa mawazo yao ikiwemo Mrisho Ngassa, wapo waliomkosoa Yondani na wapo walioichukulia ishu hiyo kama ni tukio la kawaida na mbinu za Yondani kumtoa mchezo Kwasi.

Kwa upande wa Mbwana Samatta yeye leo ameamua kupost kitu kuhusu Yondani kupitia twitter account yake na kuandika “Kelvin Yondani Cotton”

VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao

Soma na hizi

Tupia Comments