Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

PICHA: Simba SC imeambulia sare vs Asante Kotoko ya Ghana

on

Baada ya kuweka kambi kwa wiki mbili nchini Uturuki club ya Simba SC iliwasili Tanzania August 5 2018 na Jumatano ya August 8 2018 ilicheza game ya kirafiki dhidi ya Asante Kotokoto ya Ghana ikiwa ni sehemu ya kusherekea siku ya Simba Day ambayo hufanyika August 8 kila mwaka.

Simba SC ikiwa nyumbani nusura ikubali kipigo hiyo ni baada ya kuruhusu goli dakika ya 44 baada ya Owusu wa Asante Kotokoto kufunga goli la kuongoza, Simba ililazimika kusubiri hadi dakika ya 76 kupitia kwa Emmanuel Okwi ili kufunga goli la kusawazisha.

Upepo ulionekana kubadilika zaidi kiasi cha mashambulizi ya Simba SC yakafanikiwa kuzaa matunda baada ya kufanikiwa kupata penati lakini Adam Salamba akakosa, hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yalikuwa 1-1, Simba sasa wanasubiri kucheza game ya ngao ya jamii August 18 dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

“Nimeenda chumbani kwa Canavaro, alichonijibu SINTOSAHAU”-Edo Kumwembe

Soma na hizi

Tupia Comments