Michezo

Kauli ya Maradona inadaiwa kuanza kumpa presha kocha wa Argentina

on

Usiku wa June 21 2018 mchezo uliokuwa umechukua headlines sana katika World Cup 2018 ni mchezo kati ya Argentina dhidi ya Croatia ambapo ulimalizika kwa Croatia kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Argentina.

Baada ya kipigo hicho imeanza kutawala kauli ya mkongwe wa zamani wa Argentina Diego Maradona aliyoitoa siku tatu nyuma kabla ya mchezo wa Argentina na Croatia kuwa kocha wa Argentina Sampaoli kama atapoteza mchezo ujao dhidi Nigeria asirudi Argentina.

“Nigeria ni vijana na wapo fasta wanacheza mchezo wa kushambulia kwa kushitukiza lakini sijui atapokelewaje Argentina kama akishindwa kuifunga Croatia na Nigeria na kuiwezesha Argentina kufuzu 16 bora ya World Cup 2018”>>>> Maradona

Pamoja na kauli hiyo aliyoitoa Maradona anakiri kuwa kazi rahisi kwa Argentina kupata ushindi dhidi ya Nigeria katika game ya mwisho, moja kati ya vitu vinavyodaiwa kuwa vitamuweka matatizono Sampaoli ni pamoja na kuwaacha baadhi ya wachezaji katika World Cup.

FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments