Michezo

Polisi wamekamata watu saba, kisa Aubameyang wa Arsenal

on

December 2 2018 Arsenal waliibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019, mchezo huo ulikuwa na mvuto na presha ya hali ya juu kutokana na kuzikutanisha timu za jiji moja zote zikitokea London.

Wakati wa mchezo huo uliomalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa magoli 4-2, goli la kwanza lilifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang kwa penati dakika ya 10 lakini wakati anaelekea kushangailia goli hilo kulitokea kitendo cha kibaguzi kwa shabiki wa Tottenham kumrushia maganda ya ndizi mchezaji huyo.

Kitendo hicho cha kibaguzi baada ya kutokea washukiwa saba walikamatwa na Polisi lakini club ya Tottenham pia imepanga kuwaadhibu  kwa kumfungia japo hawajasema kwa muda gani, hii sio mara ya kwanza kwa wachezaji kukutana na changamoto hiyo aliwahi kukutana nayo pia Dani Alves alipokuwa FC Barcelona.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments