PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Wakala wa Toure anachekelea kipigo cha Man City?

on

Wakala wa mchezaji wa zamani wa Man City Dimitry Seluk amechukua headlines baada ya kudaiwa kuonesha ishara ya kufurahia kipigo cha magoli 2-1 cha Man City dhidi ya Lyon katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad.

Man City jana alicheza game yake ya kwanza ya hatua ya Makundi ya michuano ya UEFA Champions League akiwa nyumbani na kufungwa magoli 2-1, hivyo baada ya kupoteza mchezo huo wakala wa Yaya Toure  anayejulikana kwa jina la Dimitry Seluk amepost katuni na matokeo hayo katika twitter account yake kitu ambacho kinaashiria kufurahia kipigo hicho.

 

Ugomvi wa wakala wa Toure na kocha wa Man City Pep Guardiola ulianza baada ya wakala huyo, kumtuhumu Pep Guardiola kumtenga Toure kitu ambacho kilipelekea kumuacha baadae na sasa Toure yupo Ubelgiji akicheza soka katika club ya Olympiacos.

 

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments