Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Difaa El Jadid ya Msuva kazi kwao sasa wamewashindwa TP Mazembe

on

Baada ya siku kadhaa kupita toka club ya Difaa El Jadid ya Morocco kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya Makundi dhidi ya Entente El Setif nchini Algeria na kuambualia point moja wakiwa ugenini, usiku wa May 15 ilikuwa ni zamu yao tena kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi B dhid ya TP Mazembe.

Difaa El Jadid ya Morocco inayochezewa na mtanzania Simon Msuva usiku huo ilikuwa nyumbani kucheza mchezo wao wa pili wa club Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Jadid wakiwa nyumbani wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 2-0, Mazembe wakijipatia magoli dakika ya 53 kupitia kwa Malanco na Abdoulaye dakika ya 61.

Pamoja na kuwa Difaa El Jadid walikuwa nyumbani na wamefanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 54 dhidi ya TP Mazembe waliokuwa wana utawala mchezo kwa asilimia chache, TP Mazembe imeonekana uzoefu kuwabeba zaidi TP Mazembe kutokana na kucheza kwa mbinu zaidi huku wakitumia vizuri nafasi zao chache walizozipata na kupata ushindi.

Difaa El Jadid sasa kazi kwao watahitaji kupata matokeo mazuri katika mechi zao nne zilizosalia ili wamalize walau nafasi ya pili na wasonge mbele.

Aliyoyasema Samatta ameyatimiza, tutamuona Europa League 2018/19?

Soma na hizi

Tupia Comments