PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Taarifa kutoka hospitali kuhusu hali ya jicho la Firmino leo

on

Baada ya kuumizwa vibaya jichoni kwa kiungo wa kibrazil Robert Firmino anayeichezea Liverpool wakati wa mchezo dhidi ya Totteham Hotspurs uliyochezwa uwanja wa Wembley leo, Robert Firmino alipelekwa hospitali London mapema ili kupatiwa matibabu.

Firmino wakati wa mchezo wa Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspurs uliyomalizika kwa Liverpool kupata ushindi wa magoli 2-1, Firmino alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kutolewa nje dakika ya 74 kutokana na kuingizwa kidole jichoni na Jan Vertonghen wa Tottenham Hotspurs wakati wakiwania mpira.

Good News kwa mashabiki wa Liverpool ni kuwa mchezaji huyo tayari ameruhusiwa hospitali na jicho lake imeripotiwa kuwa limepata madhara kidogo kwa kupata mkwaruzo mdogo ambao sio wa kudumu katika jicho lake la kushoto lililokuwa limetiwa kidole naΒ Jan Vertonghen.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments