Burudani

Dogo Janja kwa wanaokosoa idea ya kujitumia kama video vixen

on

Siku tatu baada ya muimbaji wa Bongofleva Dogo Janja kuachia video yake mpya ya ‘Wayu Wayu’ maneno yalikuwa mengi mtandaoni na watu kuanza kukosoa idea yake ya video hiyo kujitumia mwenyewe kama video vixen na kuvaa mavazi ya kike.

Idea hiyo ni ngeni kuwahi kutumiwa kwa Dogo Janja na baadhi ya watu wameikosoa na kuhoji kwa nini Dogo Janja avae nguo za kike, leo kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe flani unaotafsirika kama ni kujibu wanaomkosoa.

Dogo Janja ameandika maneno haya katika picha ya aliyoipost instagram “Vyenye mi hupokea taarifa za marapa walionipa jina la RAPPA MVAA SKETI😏… #wayuwayu link in my bio”>>> Dogo Janja

Ulipitwa na gumzo mtandaoni, Dogo Janja kapaka lipstick kavaa nguo za kike??

Soma na hizi

Tupia Comments