DSTV


Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Uzalendo Kwanza imekaa kisiasa? Steven Nyerere kafunguka

on

Wiki kadhaa zimepita toka wasanii wa filamu Tanzania wakiungana na watu mbalimbali kutoka tasnia tofauti, waunde umoja wao wa Uzalendo Kwanza, wakieleza kuwa lengo la umoja huo ni kutembea Tanzania nzima kuhamasisha watanzania kupenda vya kwao.

Baada ya Uzalendo Kwanza kuenea na kuchukua headlines kwa kitendo chao cha kutoa msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya Tsh milioni 29 jijini Tanga, AyoTV imempata mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steven Nyerere na kueleza na kujibu wanaosema Uzalendo Kwanza imekaa kisiasa.

“Nataka niwakanye na hili huwa nalikanya sana nataka kusema kwamba kwenye vitu muhimu vya nchi  ambavyo vinatufanya tucheke, vinatufanya tukae na familia zetu kwa furaha tusiingize siasa kabisa, siasa ina wakati wake na wakati wake ukifika hauepukiki, Uzalendo Kwanza haina siasa”>>> Steve Nyerere

KAMA ILIKUPITA HII: Wasanii wa Uzalendo Kwanza wametoa Tsh Milioni 29 Bure!!! kwa ajili ya Tanga

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement